Ningependa sana watawala wetu wafike Addis Ababa wakiwa na macho yaliyofunguka tayari kwa kuona na kujifunza. Kwa siku takriban sita nimekuwa, kwa mara nyingine, nikivinjari jiji hili na kujionea maajabu wanayoyafanya wananchi wa Ethiopia na serikali yao, hususan katika ujenzi wa barabara, nyumba za kuishi na majengo ya ofisi. Ni maajabu matupu kwa mtu aliyeujua mji huu kihistoria.
Mara ya kwanza kwangu kuliona jiji hili ilikuwa ni Januari 1970. Nilikuwa mwanafunzi wa UDSM, mwaka wa kwanza, na nikapata fursa ya kuwakilisha jumuiya ya wanafunzi katika mkutano wa “UN Decade of Africa’s Development” uliohusisha jumuiya za kiraia na vyama visivyokuwa vya kiserikali. Nilipata nafasi ya kuutembelea mji huu na kujionea jinsi ulivyokuwa mchafu na usdiopenedeza sana. Tangu wakati huo nimekuwa nikirejea Addis mara kwa mara katika kipindi chote cha miaka 40 ‘ushei’. (more…)