Tunaanza kuona ishara za kuvurugika kwa amani kunakosababishwa na watu fulani wenye nia mbaya na taifa hili na wanaotaka kutumia uhasama wa kidini kupandikiza chuki miongoni mwetu.
Viongozi wa dini wanashambuliwa (wawili wameuawa tayari), kumekuwapo na mabishano juu ya nani ana haki ya kuchinja nyama kwa ajili ya biashara, na malumbano mengi mno yasiyo na tija yo yote kwa taifa. Watu wameanza kuangaliana kwa mtazamo wa “Huyu ni wa dini gani?” Nchi yetu inakabiliwa na hatari ya kweli ya kusambaratika au kuingia katika zahma kuu. (more…)