Mitindo huja na kupita, na mara nyingi huondoka bila kuacha makovu ya kudumu, na kwa hiyo huwa inavumilika. Lakini mtindo huu wa dadaz etu kuvaa nywele za wengine unaibua maswali mengi, hata kwa kimi ambaye sina chembe nyingi za uhafidhina.
Kitendo cha kuvaa nywele zilizoingizwa kutoka nje, bila kujua kama zilinyolewa kutoka maiti, au zilinunuliwa kwa binti wa Kihindu aliyekuwa akifanyiwa tohara ya ibada, au ni manyoya ya kondoo, kinasikitisha na kusononesha kwa sababu kinaonyesha jinsi tunavyojidharau kama Waafrika. (more…)